Kesi ya utakatishaji dola milioni 6 ambazo ni zaidi ya Tsh. bilioni 13 inayomkabili Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya na wenzake, imeahirishwa hadi July 28, 2017 kutokana upande wa mashtaka kusubiri vielelezo vya awamu ya pili vya ushahidi kutoka Uingereza.
Kesi ya utakatishaji fedha dola mil.6 inayomkabili Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA Harry Kitilya na wenzake, imeahirishwa hadi July 28, 2017. pic.twitter.com/MT64YKzwkO
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Mbali ya Kitilya, wengine ni mshindi wa Mashindano ya Urembo (Miss Tanzania), mwaka 1996, Shose Sinare na Mwanasheria wa benki ya Stanbic, Sioi Solomon kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka nane.
Wakili wa serikali, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hadi wakipata vielelezo muhimu kutoka Uingereza
VIDEO: Umepitwa na uchambuzi wa Magazeti ya leo July 14, 2017? Bonyeza play hapa chini kutazama.