Hii ni ajali ambayo imetokea njia Panda ya kwenda Arusha kama unatokea Singida, wakazi wa eneo hilo wamechoma moto basi la Mtei ambapo millardayo.com imeongea na miongoni mwa mashuhuda na abiria wa ajali hiyo na wametoa haya maelezo hapa chini.
Abiria mmoja ana sema ‘tumepandia pale stand ya Mwenge tulikua tunaenda Arusha na tulipofika hapa kuna abiria akasema kuna watu wamegongwa ndo tukashuka tukakuta kweli wamegongwa watu wanne hii pikipiki ilikua mbele alikua kapakia abiria watatu na yeye mwenyewe alikua wanne tulikua tunaongozana nae akataka kumpita akaona basi mbele linakuja akarudi akataka kumuova teki huyu dereva bodaboda’
‘Wanakijiji ndio wakapigiana simu wakaja hapa ndio wakasema tulichome moto hili basi leo’
Kamanda wa Polisi Singida anasema ‘abiria wawili wa pikipiki walipoteza uhai papohapo na abiria wawili waliumia na kukimbizwa hospitalini mpaka sasa taarifa tulizonazo ni kwamba abiria mmoja ambaye alikua amejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu hivyo jumla ya waliofariki ni watatu’
‘basi hilo limeteketea sehemu ya juu yote ya kukaa abiria na sehemu ya chini imeharibika kutokana na joto ambalo lilikuwa linatokea juu, tukio limetokea leo saa moja asubuhi katika kitongoji cha Ijanuka kijiji cha Kisasida’
Basi hili mali ya kampuni ya Mtei lenye namba za usajili T.742 ACU aina ya Scania lilikua likiendeshwa na Dismas Ludovick na lilikuwa linatoka Singida mjini kwenda Arusha mjini.