Hii ilikua ni kwenye mkutano ulioandaliwa na Wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali Tanzania wakiwemo wa Kariakoo ambao waliamua kufunga maduka yao Alhamis January 9 2014 kwa ajili ya kukutana na Waziri wa Viwanda na biashara Karimjee hall kueleza kero zao kuhusu kodi za mashine za T.R.A.
Kabla ya Waziri kuzungumza nao vizuri, kuwatuliza na kuwapa ahadi ya malalamiko yao kufanyiwa kazi… kuna baadhi ya Wafanyabiashara walinyanyuka na kuyasema ya moyoni, alichokisema huyu Mwanamke kutoka Kilimanjaro kilimtofautisha na wengine wote waliotoa maoni.
Kwanza aliyatoa kwa hisia, alichambua na kueleza kila kitu cha moyoni >>>> anaitwa Neema Urassa na unaweza kumsikiliza kuanzia mwanzo mpaka mwisho hapo chini.
Mimi ni mmoja kati ya wanawake walioanza biashara wakiwa na umri mdogo mimi nmeanza biashara toka darasa la nne, naomba nitoe maoni yangu ambayo nimeona kama leo nisingeongea nisingelala, kodi ya Tanzania ukitaka kuichunguza iko kwenye makundi 8′
‘Kodi ya nyumba, Kodi ya duka, mzigo unaoleta unakatwa kodi, makadirio ya mwaka unakatwa kodi, bado mnatuambia na mashine……. hivi hizo kodi tunazolipa tutalipa ngapi jamani, unaweza kujikuta unalipa zaidi ya milioni 20 huku umechukua mkopo wa milioni 40 unajikuta umefanyia kazi mkopo na kodi’
‘Angalia nchi ndogo kama dubai imeanza maendeleo juzi mwaka 1994, Dubai wanachajiwa kodi wafanyabiashara wote ndo maana ukienda kununua mzigo kila mfanyabiashara anakuuliza lete Risiti’
Hizi hapa chini ni dakika dakika 4 za huyu dada alivyoongea kwa uchungu kwenye mkutano wa wafanyabiashara uliofanyika Diamond Jubilee leo.
Bonyeza play kusikiliza.
January 9 2014 Wafanyabiashara wa mikoa mbalimbali Tanzania wakiongozwa na wa mkoa wa Dar es salaam waliandaa mkutano wao wenye nia ya kuishinikiza serikali kutoa mashine za Efd zilizo chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania T.R.A kwenye mkutano huu Mgeni Rasmi akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.Abdallah Kigoda.
Katika risala iliyosomwa mbele ya Mgeni rasmi Mh Kigoda, wafanyabiashara hao walikumbushia waraka wao juu ya kero zao za mashine za kieletroniki za Efd, wakidai mfumo wa mashine hizo haufanyi kazi kwa ufanisi na kwamba unatoa nafasi za maafisa mbalimbali wa polisi wasiokuwa waaminifu kuingia na kuona hilo ni dili.
Mbali na hayo, Wafanyabiashara hao wamewazungumzia maafisa wa polisi wanaotembea na pikipiki maarufu kama kero kwao kwa kufanya mashine za Efd kuwa sehemu ya kujiingizia kipato ambapo imekua wakiona mfanyabiashara yoyote amebeba mzigo wanamsumbua.