Kwenye Magazeti ya Tanzania leo Jluy 25, 2017 issue mbalimbali zimechukua headlines ambapo miongoni mwao ni kuhusu Mkazi mmoja wa Kyela, Mbeya Erick Mwangonda kuuawa kwa risasi na watu wasiofahamika akiwa kwenye banda lake la biashara.
Mwendesha Bajaj mkazi wa Njoro, Moshi ameuawa na mwili wake kufukiwa nyuma ya nyumba ya mtuhumiwa wa mauaji hayo wilayani Siha, Kilimanjaro.
IGP Sirro amewaagiza Askari na Maafisa wa Jeshi hilo kuwa na utendaji bora wa kazi unaofuata maadili, kanuni na sheria. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Wanachama 41 wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Kijana Mwesigwa Mberwa amekutwa amekufa chumbani ktk nyumba ya kulala wageni Mlandizi, Pwani ikiwa ni siku 4 tangu awasili hapo. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Rais JPM amesema ataendelea kuteua wanachama wa Vyama vya Upinzani kwenye Serikali yake ili wafanya kazi kwa ajili ya Watanzania. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Imeelezwa chanzo cha mwandishi kumpiga risasi baba mkwe wake ni hisia kuwa alisababisha kuvunjika ndoa yake miaka 10 iliyopita. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Rais mstaafu JK amesema kuzungumza ktk majukwaa ya kisiasa kuwa kupeleka watu nje ya nchi kutibiwa ni kupoteza fedha sio uhalisia #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Mwanamke mmoja mkazi wa Mwanshinga, Mbeya na wanawe wawili wamemwagiwa maji yanayosadikiwa kuwa tindikali kwa sababu za kimapenzi #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Mwanafunzi mmoja wa Shule ya Atlas amekutwa amekufa katika mazingira yanayotatanisha ikidaiwa alibakwa kisha kunyongwa. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
TRA imeitaka Acacia kulipa zaidi ya Tsh. 424tril kwa kukwepa kodi tangu mwaka 2000 ambazo ni sawa na Bajeti ya Tanzania miaka 13. #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Mwendesha Bajaj mkazi wa Njoro, Moshi ameuawa na mwili wake kufukiwa nyuma ya nyumba ya mtuhumiwa wa mauaji hayo wilayani Siha. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Rais JPM leo ataanza ziara ya kikazi mkoani Singida ambako atazindua Barabara ya Manyoni, Itigi hadi Chaya yenye urefu wa km 89.3. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Mwanachama wa CCM Tawi la Khadija Binti Kamba, Ilala DSM amekimbia na daftari la majina ya wanachama wanaostahili kupiga kura #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Mkazi mmoja wa Kyela, Mbeya Erick Mwangonda ameuawa kwa risasi na watu wasiofahamika akiwa kwenye banda lake la biashara. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Serikali za Tanzania na Kenya zimekubaliana kuondoa vikwazo vilivyokuwa vikiikabili sekta ya biashara baina ya nchi hizo. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Rais JPM amesema atabomoa nyumba hata za Mawaziri ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa kutoka D'Salaam, Mwanza hadi Kigoma. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Mbunge Tundu Lissu amerudishwa rumande baada ya kusomewa shtaka moja la kutoa lugha ya uchochezi na kunyimwa dhamana. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Imeelezwa kuwa umasikini haukwisha nchini kama Wanawake hawataendelea kupambana ktk ujasiriamali, kilimo, uvuvi na mifugo. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
M/kiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili Prof. Lipumba amewafuta uanachama Wabunge 8, Madiwani 2 kwa madai ya kukihujumu chama #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Waziri wa Habari, Dr. Mwakyembe ameiongezea muda wa siku 10 Kamati ya kuchunguza mkataba wa ubia kati ya TBC na StarTimes. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Serikali imeitaka Benki ya NMB kulipa kodi ya ardhi Tsh. 72m ambazo ilishindwa kuilipa H'shauri ya Jiji la Mwanza tangu 1997. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
Wakazi wawili wa Ubungo Kibangu, DSM wamefikishwa Mahakamani wakikabiliwa na kesi ya kuiba mifugo yenye thamani ya Tsh. 12.4m #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 25, 2017
ULIPITWA? Alichozungumza mke wa Lissu baada mume wake kukosa dhamana…PLAY kwenye VIDEO hii kutazama!!!
ULIPITWA? “Matatizo yaliyopo kwenye uwezo wa Kiongozi na hakuyatatua, nalala mbele na huyo Kiongozi” – JPM