Mbunge kutoka mkoa wa Singida, Mwanasheria wa CHADEMA ambae pia ni Rais wa TLS Tundu Lissu bado yupo kwenye headlines za Mahakama.
Leo August 7/2017 Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imempa onyo la mwisho Tundu Lissu kuhakikisha anafika katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mahakamani hapo.
Onyo hilo limetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya wakili wa serikali Mutalemwa Kishenyi kudai shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini mshtakiwa Lissu hajafika Mahakamani.
Wadhamini wa Lissu hawakufika pia Mahakamani huku Wakili wa Lissu Jeremiah Ntobesya amedai kuwa mteja wake ana udhuru ambapo baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mwambapa amesema hii ni mara ya pili Lissu hajafika katika kesi hiyo hivyo anatoa onyo la mwisho ahakikishe anafika.
Hakimu huyo amesema kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa ambapo baada ya maneno hayo ameahirisha kesi hiyo hadi August 14/2017.
Katika kesi hiyo ya uchochezi (Dikteta uchwara) Lissu anadaiwa alitenda kosa hilo July 28/2016 katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Ilala Dar es Salaam.
VIDEO: Rais Magufuli afunguka, ni kuhusu kutawala miaka 20… bonyeza play hapa chini kutazama
ULIPITWA? Majibu ya Lissu kuhusu kumfuta uwanachama Waziri Mwakyembe, play hapa chini kutazama
VIDEO: “Utaratibu unafanywa wa kumpeleka Edward Lowassa Mahakamani” – Tundu Lissu, play hapa chini kujionea zaidi
VIDEO: Tundu Lissu alivyogoma kutoka Mahakamani ili asikamatwe na Polisi, tazama hapa chini kwenye hii video