Mkoani Iringa leo basi moja lanusurika kuwaka moto na daladala moja yateketea yote kwa moto wakati wanafunzi wa masomo ya kuunga vyuma katika gereji bubu eneo la uwanja wa Samora mjini Iringa wakijifunza kuunga ngao ya daladala hiyo yenye namba za usajili T189 AWN .
Tukio hilo limetokea leo majira ya 8 na dakika 15 mchana wakati vijana wawili wanaojifunza kuunga vyuma wakiendelea na mafunzo ya kuunga ngao ya daladala hilo.
Mmoja kati ya wafanyakazi wa gereji hiyo Filibert Mwihava amesema kuwa chanzo cha daladala hilo kuwaka moto ni vijana wawili ambao wanajifunza ufundi wa kuunga vyuma katika eneo hilo kufanya kazi hiyo bila kuzingatia kanuni ya kazi hiyo.
Kanuni hizo ambazo vijana hao walikosea amezitaja kuwa ni pamoja na kuunga ngao ya nyuma ya daladala hilo wakiwa jirani na tenki la mafuta hivyo kutokana na cheche zilizokuwa zikitoka zilisababisha moto kuibuka kwa kasi .
Mwihava amesema katika moto huo kushika daladala hiyo inayofanya safari zake kati ya Tumaini na Zizi la Ng’ombe mjini Iringa hakuna mtu aliyezulika zaidi ya basi lenye namba za usajili T 457 AMQ kutetekea upande wa mbele kabla ya kuokolewa .
Kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoani Iringa walifika kwa wakati na kufanikiwa kuzima moto huo ambao pengine ungeweza kusababisha madhara makubwa katika eneo hilo lenye ofisi ,maduka ya watu waliojenga kuzunguka uwanja huo wa Samora.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kiongozi wa askari wa zimamoto ambao walifika eneo hilo John Zacharia amesema kuwa kuwa chanzo cha moto huo ni uzembe wa ofisi hiyo.
Source:http:www.matukiodaima.com