Hali ya sintofahamu imetawala katika Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 29, 2017 baada ya Mawakili kususia shughuli za Mahakama ambao itakuwa kwa siku mbili mfululizo.
millardayo.com imefika katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kushuhudia baadhi ya Mawakili wakihudhuria katika shughuli za Mahakamani kama kawaida.
Hata hivyo, shughuli za Mahakama zinaendelea kama kawaida ingawa idadi ya Mawakili waliofika katika Mahakama hizo ni ndogo ikilinganishwa na siku nyingine.
Mmoja wa Wakili wa kujitegemea ambao wameonesha kwenda kinyume na maazimio ya Baraza la Uongozi wa TLS, Jerome Msemo anasema hawezi kugoma kwa sababu hakuna kifungu kinachomtaka Mwanasheria au Wakili agome.
>>>”Nina wateja wangu ambao nimeingia nao mikataba, nisipofika Mahakamani itakuaje? Hakuna sababu ya msingi ya kugoma.”
Wakili Fredrick Jonathan naye amesema kulipuliwa kwa ofisi za Mawakili za IMMMA ni tukio la kulilaani lakini sio kwa mfumo wa mgomo akidai kuwa ana wateja ambao wapo Mahakamani na hawahusiki na mgomo huo hivyo kugoma kwake kungewaathiri.>>>”Sijaona kama ni busara kugoma kwani tukigoma ndio itasaidia wahalifu wakamatwe?”
ULIPITWA? TUNDU LISSU APINGWA: Wakili Manyama kaongea hadharani…
MBUNGE MSUKUMA: Kamjibu tena Lissu kuhusu mgomo wa Mawakili