Kila mtu ana ndoto ya kuwa na kazi nzuri na mara nyingi huchagizwa pale unapofikia kiwango fulani cha elimu na kutamani ufanye kazi katika kampuni kubwa kutokana na kuvutiwa na makampuni hayo.
Sasa leo ninayo hii stori ambapo unaambiwa makampuni makubwa ya teknolojia na Uhasibu inatawala katika list ya waajiri ambao wanafunzi wengi wanatamani kufanya kazi huku Google na Apple zikiongoza list ya sehemu bora za kufanya kazi, kwa mujibu wa Universum.
Universum ilifanya utafiti kwa karibu wanafunzi 300,000 wanaosomea Biashara na engineering/IT katika nchi zenye uchumi mkubwa duniani: Brazil, Canada, China, Ufaransa, Ujerumani, India, Italia, Japan, Urusi, Korea Kusini, Uingereza na Marekani.
Katika utafiti huo wanafunzi wanaosoma Engineering/IT wanapenda zaidi makampuni ya teknolojia tofauti na wenzao wanaosoma biashara.
EXCLUSIVE INTERVIEW: Yvonne Darcq na Millard Ayo
Mtanzania Milionea Mtarajiwa alieacha kazi ya mshahara wa milioni 1