Zawadi kutoka MULTICHOICE Tanzania zilikuwepo siku nyingi na kinachofanywa sasa ni muendelezo tu wa kilichoanzishwa ambapo mara nyingi tumeshuhudia jinsi wanavyowazawadia wateja wao.
Leo ni zamu ya Wateja 76 wa DStv ambao wamejinyakulia zawadi mbalimbali kutoka Multichoice Tanzania katika promosheni inayoendelea ya ‘Jishindie na DStv’ ambapo mteja hupata fursa ya kujishindia zawadi kwa kulipia king’amuzi chake kwa angalau miezi miwili mfululizo.
Kati ya washindi hao, 25 wamejishindia zawadi ya ving’amuzi vya kisasa vya DStv Explora huku washindi wawili wakijishindia Kifurushi cha Premium cha Tsh 169,000 cha mwezi, wengine wawili Kifurushi cha Compact+ cha Tsh 109 000 huku washindi 10 wakishinda kifurushi cha Compact cha Tsh 69,000 na 10 wengine wakishinda kifurushi cha Famili cha Tsh 39,000 na washindi 25 wameshinda kifurushi cha Bomba cha Tsh 19,000.
Washindi wawili wa droo kubwa ambao ni Anicet Macheta wa Kagera na Hassan Juma Hassan wa Dar es Salaam wamejishindia zawadi kubwa kabisa ambayo ni safari ya kutalii Visiwani Zanzibar pamoja na familia zao zisizozidi watu wanne kila familia.
Akizungumza baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo ya mwisho leo katika Ofisi za Multichoiche Tanzania, Meneja wa Uhifadhi Wateja Hilda Nakajumo amebainisha kuwa zaidi ya wateja 30,000 wameshiriki kwenye promosheni hiyo iliyoendelea kwa miezi miwili.
Hilda amesema, wamefurahi kuona washindi takriban 200 waliopatikana wakati wote wa promosheni wametoka maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo Arusha, Mwanza, Dar es Salaam, Kagera, Iringa, Geita, Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Ruvuma na mikoa mingine kote nchini.
>>>>”Wakati wote DStv tunahakikisha kuwa wateja wetu wanafurahia huduma zetu kwani mbali na kwamba sisi ni vinara katika burudani na michezo, pia tunakuwa na promosheni za mara kwa mara ambapo wateja wetu hupata zawadi mbalimbali.”
Aidha, amesema kuwa mwaka huu ni mwaka wa neema kwa wateja wa DStv ambapo mbali na kuongeza channel kwenye vifurushi hasa vya bei ya chini, pia hivi majuzi DStv ilipunguza bei za vifurushi vyake vyote ili kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata huduma hizo kwa unafuu mkubwa.
Kampuni ya Multichoice Tanzania inayoendesha biashara ya vingamuzi vya DStv, ina umri wa miaka 20 sasa ambapo ilianza shughuli zake hapa nchini mnamo mwaka 1997.
BUNGENI! Maswali makubwa 10 siku ya kwanza Mkutano wa Nane