Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu ambaye alijeruhiwa kwa risasi jana mchana akiwa nyumbani kwake Dodoma baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana, amefikishwa katika Hospitali ya Nairobi, Kenya.
Mkuu wa Idara ya Uenezi ya CHADEMA Hemed Ali amesema Tundu Lissu aliwasili saa Saba katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi (Nairobi Jomo Kenyatta International Airport) ambapo alipokelewa na team ya Madaktari kutoka Nairobi Hospital na kumuanzishia matibabu wakiwa naye ndani ya Ambulance kuelekea Hospital.
Katika taarifa yake, Hemed Ali amesema baada ya kufikishwa Hospitali alifanyiwa vipimo na saa nne asubuhi aliingizwa theatre ambapo alifanyiwa stabilization ili aweze kukabiliana na upasuaji zoezi lililofanikiwa huku Madaktari wakieleza hakuna hali yoyote ya hatari na matibabu yake yanaendelea kwa mafanikio.
Hadi kufikia Saa Tisa Alasiri alikuwa hajatoka theatre ambapo Madaktari wameeeleza kuwa wanaendelea vizuri.
Aidha, Hemed Ali amesema hadi wakati huu hawajapata ushirikiano wowote wa ubalozi wa Tanzania uliopo Nairobi na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amezungumza na vyombo mbalimbali vya habari.
IGP Sirro kaongelea ishu ya Tundu Lissu kupigwa risasi
“Kwa yanayoendelea hakuna mwenye uhakika wa maisha” – Hussein Bashe