Top Stories

IGP Sirro kaongelea ishu ya Tundu Lissu kupigwa risasi

on

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amekutana na wanahabari kuzungumzia masuala ya ulinzi na usalama likiwepo tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

IGP Sirro amesema kuwa Jeshi la Polisi liko makini katika kufanya upelelezi kuhusu tukio hilo ambapo baadhi ya wapelelezi wazuri wameshapelekwa Dodoma katika kuongeza nguvu ya upelelezi huo.

Aidha, amesema Jeshi la Polisi litahakikisha kuwa wahusika wa tukio hilo wanakamatwa huku akiwasihi wananchi kushirkiana na Polisi kutoa taarifa muhimu zitakazorahisisha jitihada hizo.

>>>”Mheshimiwa Lissu pia ni mwanadamu na ndio maana tunapisha uchunguzi ili kujua sababu halisi za shambulio hili. Jeshi liko hapa ili kulinda Watanzania na hivyo watu watulie na wawe na amani.” – Kamanda Sirro

“Kwa yanayoendelea hakuna mwenye uhakika wa maisha” – Hussein Bashe

Soma na hizi

Tupia Comments