Kutoka Nairobi, Kenya Jumapili ya September 10, 2017 Mbunge Singida Mashariki Tundu Lissu anaendelea kupatiwa matibabu baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Nairobi kufuatia kuumizwa kwa risasi na watu wasiojulikana waliomvaniwa akiwa nyumbani kwake Dodoma September 7, 2017.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe jioni hii ametoa taarifa kuwa Mbunge huyo ameingizwa chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mwingine akisema kuwa anahitaji matibabu maalum yanayohitaki wataalam wengi, vifaa tiba maalum na gharama kubwa ambapo hadi sasa, zaidi ya Tsh. Millioni 100 zimeshatumika kuokoa maisha yake.
Mbowe amebainisha kuwa thamani ya Lissu ni kubwa kuliko kiwango chochote cha fedha hivyo watatumia kila njia iliyo halali ili kupata fedha za kutosha kumtibu ili kumrudisha kwenye uwanja wa kudai haki, demokrasia na ustawi kwa woteTanzania.
Amewashukuru Watanzania na Wabunge wote wa CHADEMA kwa namna walivyobeba gharama za awali pamoja na Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujitoa kwao kuchangia matibabu ya Tundu Lissu.
Aidha, wageni mbalimbali mashuhuri kutoka Tanzania, Afrika Mashariki na Jumuiya za Kimataifa zimekuwa zikifanya juhudi kubwa kumtembelea Lissu huku akisema ulinzi umeimarishwa katika eneo anakotibiwa na hairuhusiwi wageni kumwona hadi madaktari wakiridhika kuwa hali yake ya kimatibabu inaruhusu.
Kwa upande mwingine, Dereva Tundu Lissu, Simon Mohamed Bakari naye yupo Nairobi akipatiwa huduma za kisaikolojia kutokana na kushuhudia shambulio hivyo kusumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo.
IGP SIRRO KAPEWA MBINU MPYA KUKABILIANA NA WANASIASA
BREAKING: Watu 30 na Magari wakamatwa Dodoma, Dereva wa Lissu aitwa