Kampuni ya michezo ya kubashiri duniani ya SportPesa imeteuliwa kwenye vipengele viwili kuwania tuzo za bishara ya mpira wa miguu za nchini Uingereza zijulikanazo kama Football Business Award (FBA) ambazo zimepangwa kufanyika Novemba 2 kwenye Ukumbi wa Iconic Tobacco Dock jijini London.
Tuzo hizo ambazo zitafanyika mwaka huu kwa mara ya sita, zinahusisha jumla ya taasisi 97 zilizoingia kwenye hatua ya fainali ambazo zimegawanywa kwenye vipengele 16, SportPesa imepangwa kuwania tuzo mbili kwenye kipengele cha uhamasishaji bora wa nembo ya kampuni unaohusisha mpira wa miguu kupitia vilabu vya Everton na Hull City ambao ni washirika wao wakuu.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya SportPesa Tanzania Pavel Slavkov amepokea uteuzi huo kwa furaha
“Ni jambo la kufurahisha na kutia moyo kuona jinsi ambavyo ulimwengu unatambua jitihada za dhati za kampuni yetu ya SportPesa katika kuendeleza mpira wa miguu duniani na ndio sababu kubwa ambayo inatufanya kuweza kushindanishwa na kampuni mashuhuri duniani kama vile Nivea na Virgin Media inayomilikiwa na tajiri maarufu duniani, Sir Richard Branson,”>>> Pavel
Udhamini wa SportPesa kwa klabu ya Everton uliifanya klabu hiyo ambayo ni bingwa mara tisa wa Ligi Kuu nchini Uingereza kutembelea Tanzania katika sehemu yao ya maandalizi ya msimu mpya ikiwa ni timu ya kwanza kutoka nchini Uingereza kutembelea ukanda wa Afrika Mashariki. Wakiwa nchini Tanzania, Everton waliweza kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.
Sambamba na ziara ya Everton nchini Tanzania kuweza kuteuliwa kuwania tuzo kwenye kipengele hicho, lakini pia Kampuni ya SportPesa imeteuliwa kwenye kipengele hicho kwa mara nyingine kupitia udhamini wake kwa klabu ya Hull City ambayo tayari imeshafanya ziara mbalimbali nchini Kenya pamoja na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya nyota wa Ligi Kuu ya Kenya iliyopigwa Februari mwaka huu.
Huu utakuwa ni uteuzi mwingine kwa kampuni ya SportPesa kuwania tuzo za kimataifa baada ya miezi mitatu iliyopita kutwaa tuzo mbili kwenye tuzo za Discovery Sports Industry Awards zilizofanyika jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.Katika tuzo hizo, SportPesa ilinyakua tuzo kwenye kipengele cha kampeni bora ya kimasoko ya “Made Of Winners” kwa nchi za Afrika sambamba na Udhamini bora kupitia mashindano ya Super 8.
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0