Asasi isiyo ya Kiserikali ya EngenderHealth kwa kushirikiana na Bloomberg Philanthropies, Fondation H&B Agerup na CDC wamekabidhi vituo vya afya 26 mkoani Kigoma, vituo hivyo vya afya vinatarajiwa kuinua upatikanaji wa huduma za afya na kuokoa maisha ya watu wengi hasa akina mama wanaojifungua.
Katika vituo 26 vilivyokabidhiwa, 24 ni vipya na viwili vimefanyiwa marekebisho, Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vituo hivyo, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamis Kigwangalla amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwani havikubaliki ambapo alitoa wito kwa akina Mama kuwahi mapema kliniki pindi wanapojihisi wajawazito kwa kuwa vifo vingi vinaepukika kama mama ataanza kuhudhuria kliniki mapema.
Ulikosa hii? WAZIRI UMMY! “Hatukatazi Watumishi wa Afya kumiliki maduka ya Dawa lakini…”, Bonyeza play hapa chini kutazama