Siku 14 sasa zimepita tangu Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu apigwe risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Dodoma kisha kupelekwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Nairobi Kenya huku watu wa jamii mbalimbali wamekuwa wakihamasishwa kuchangia huduma za matibabu yake.
Watu mbalimbali wameendelea kumtembelea Lissu Hospitali kumjulia hali na miongoni mwao ni Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu ambaye kupitia account zake za Twitter na Facebook ameeleza kuwa wanasubiri ripoti ya Madaktari kujua mwenendo wa matibabu ili kuwapatia madaktari bingwa wa Marekani.
Tumekuwa #NairobiHospital tukisubiri MADAKTARI watoe RIPOTI ya mwenendo wa MATIBABU ya Mh #TunduLissu kwa minajili ya kuwapatia MADAKTARI BINGWA wa Marekani na kuona uwezekano wa Mh #TunduLissu kupatiwa RUFAA kwa matibabu zaidi NJE., LAKINI bado KALAMU zao ni nzito kuandika RIPOTI hii siku ya tatu tangu tuahidiwe.
Binafsi, nimerudi NAIROBI tangu JANA kushiriki maandalizi ya uwezekano wa kumhamishia Mh #TunduLissu Marekani kwa ajili ya huduma yenye ubora zaidi, endapo MADAKTARI wa #NairobiHospital wangeridhia. Kesho asubuhi nitarejea hospitalini kusikiliza kauli ya mwisho ya MADAKTARI kuhusu RIPOTI hiyo.
NAIROBI HOSPITAL: Tundu Lissu aonyesha uso wa tabasamu
TUNDU LISSU ASIMULIA: Anavyofatiliwa na gari asilolijua…. bonyeza play hapa chini kumtazama
BREAKING: Mipango ya kumpeleka Tundu Lissu Marekani imesimamishwa, play hapa chini kupata stori kamili.
HUTAKI KUPITWA??? Kama una simu ya ANDROID jiunge na APP MPYA ya ‘millardayo‘ kwa kubonyeza HAPA HUTAKI KUPITWA NA BREAKING NEWS??? Jiunge na Youtube, Twitter, Instagram na Facebook za ‘millardayo‘ kwa kubonyeza hapa >>> Youtube HAPA, Twitter HAPA, Instagram HAPA, Facebook HAPA