Mtahiki wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesitisha Mkataba wa Kampuni ya Ukamataji Magari Wilaya ya Temeke ya Mwamkinga Action Mart kutokana na kukamata magari kwa kuvizia.
Mwita amesema kumekuwa na changamoto katika jiji la Dar es Salaam kuhusu suala la ukamataji wa magari, ambapo suala hilo lipo chini ya Jiji.
>>>”Kadri siku zinavyokwenda hali inakuwa mbaya na wanaomiliki magari wanateseka. Niliwahi kuongea kwamba wakandarasi waheshimu wenye magari.”
Aidha, Mwita amesema wameamua kusitisha Mkataba na Kampuni hiyo, kwa sababu anakamata malori kwa kuwaotea, hivyo amesitisha mkataba wake tangu September 18, 2017.
>>>”Hivyo haiwezekani mtu kapaki kidogo anapigwa cheni. Kuanzia leo Mkandarasi Mwamkinga tumesitisha mkataba wake na aache kufanya kazi yotote. Pia wengine wasipobadilika tutaendelea kufuta mikataba, kwani kanuni inasema si chini ya dakika 30 lakini mtu akipaki gari kidogo tu anakamatwa.”
ULIPITWA? Maamuzi Mapya ya Meya DSM kuhusu Machinga Complex
Gari la kubebea miili ya marehemu waliokosa ndugu DSM lililozinduliwa…