Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzanai ‘TFF’, Jamal Malinzi na wenzake wanaokabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418 wanaendelea kusota rumande baada ya kesi yao kuahirishwa kwa sababu ya kutokamilika upelelezi.
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi October 5, 2017.
Mbali ya Malinzi, washitakiwa wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa Shirikisho hilo, Nsiande Mwanga ambao wanakabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.
UKALI: Mkuu wa Mkoa aagiza Dereva azunguke na Ambulance bila Mgonjwa