Naibu Spika Dr Tulia Ackson amefanya ziara mbalimbali mkoani Mbeya ambapo Jana September 20, 2017 aliongozana na baadhi ya wadau wa elimu hadi shule ya Sekondari Ikuti iliyopo Wilaya ya Rungwe mkoani hapo kwa ajili ya kuendesha harambee ya ujenzi wa hosteli na ukumbi wa wanafunzi shuleni hapo.
Katika harambee hiyo zaidi ya shilingi milioni thelathini zilipatikana huku ahadi nyingine zikitolewa ikiwemo ya mdau wa elimu Ndele Mwaselela alitoa ahadi ya kusomesha wanafunzi watato ambao ni yatima hadi watakapofika chuo kikuu.
Kwa upande wake Dr Tulia ameeleza kuna wananchi wengine wanakataa kuchangishwa michango mbalimbali ya shule kwa kudai kuwa serikali imeahidi elimu bure jambo ambalo siyo sahihi kwani serikali inagharamia ada ya elimu na wananchi ni lazima wachangie miundombinu ya shule.
Uliikosa hii? BUNGENI: Maswali makubwa 7 siku ya mwisho Mkutano wa Nane
Hii je? “Wabunge tuwe makini na usalama wetu…” – Spika Ndugai