Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo amefika katika Kata ya Sekei ambako kumezuka moto na kuteketeza nyumba za Polisi usiku huu ambapo familia 13 za Polisi zenye jumla ya watu 44 zimekosa mahala pa kulala kutokana na nyumba zao kuteketea kwenye moto huo.
RC Gambo ameagiza utaratibu ufanyike haraka kuhakikisha familia hizo zinapatiwa mahala pa kulala usiku huu huku utaratibu mwingine ukiendelea kufanyika.
#ARUSHA Familia 13 za Polisi zenye watu 44 hazina pa kuishi baada ya moto uliozuka Line Polisi kuteketeza nyumba zao. #MillardAyoUPDATES. pic.twitter.com/BvwsH2WsPp
— AyoTV (@ayotv_) September 27, 2017
Waziri Nchemba karudi Jimboni kwake na maamuzi mapya