Uchaguzi uliotakiwa kufanyika November 2016 nchini Congo na baadaye kuahirishwa hadi kuelekea mwishoni mwa mwaka huu, umeahirishwa tena na Tume ya Uchaguzi nchini humo mpaka kufikia April 2019.
Sababu ya mabadiliko haya kwa mujibu wa tume hiyo ni machafuko yanayoendelea katika mji wa Kasai ambao unachelewesha kukamilika kwa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura na hivyo itaihitaji tume hiyo kutumia siku 504 kujiandaa na uchaguzi huo.
Mabadiliko haya yanahofiwa kuweza kuleta machafuko zaidi nchini humo, ikiwa vyama vya upinzani pia vikishinikiza Rais Joseph Kabila kuachia madaraka hayo ambayo ameyashikilia tangu mwaka 2001 aliuawa baba yake Laurent Kabila aliyekuwa rais.
Ulipitwa na hii? Baraza Jipya la Mawaziri laanza kazi rasmi