Raia wa Denmark, Ricki Thomason mwenye umri wa miaka 46, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo October 13, 2017 akikabiliwa na kosa la kukutwa na nyara ya Serikali ambayo ni Fuvu la Nyumbu lenye thamani ya Tsh. Milioni 1.
Raia huyo amesomewa kosa lake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.
Kishenyi amedai mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la kukutwa na nyara ya Serikali ambayo ni Fuvu la Nyumbu likiwa na thamani ya Tsh. Milioni 1,460,108.
Inadaiwa mshtakiwa alitenda kosa hilo katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, October 9, 2017 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyama Pori.
Baada ya kumsomea kosa hilo, Kishenyi amedai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali (PH).
Hata hivyo, Hakimu Mkeha alimpa masharti ya dhamana mshtakiwa huyo, ambapo ametakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Tsh. Milioni 20, pia awasilishe hati yake ya kusafiria (Passport).
Kesi hiyo imeahirishwa hadi October 16/2017.
MWANZA: Akamatwa akijifanya mtumishi wa Jiji na kukusanya ushuru