Tumekuwa tukiona baadhi ya Mastaa wakichora tattoo kama mapambo katika miili yao au tamaduni zao ambapo wengi huchora vitu ambavyo huvipenda au vyenye kumbukumbu zao.
Muimbaji Cassie wa Marekani ambaye ni Mpenzi wa siku nyingi wa Nguli P Diddy ameamua kuchora tattoo ya ramani ya Afrika katika mwili wake na kuonyesha mapenzi yake kwa Bara la Afrika.
Kama haufahamu Cassie alizaliwa 1986 New London Baba yake akiwa na asili ya UFilipino na Mama yake ni Mmarekani mwenye asili ya Afrika, Mexico na India Magharibi hivyo inawezekana kuchora kwake kwa tattoo ya Afrika katika mwili wake inatokana na mapenzi ya asili alipotokea mama yake.
“Tuache roho za kikoloni akiachia ngoma Vanessa unajikausha” – Vanessa Mdee
IMEFAHAMIKA: Hapa ndipo anapoishi Dr. Luis Shika, Majirani waongea