Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kiongozi wa Twanga Luiza Mbutu mazishi ya MCD ilikuwa yafanyike leo saa 10 jioni, lakini familia imekubali kusogeza mbele ili wafanyakazi wenzake pamoja na marafiki wa marehemu waweze kuwahi mazishi hayo ya aliyekua mpiga tumba wa Twanga pepeta Mcd.
Msafara wa waimbaji wa Twanga pepeta,wawakilishi wa bendi zingine,wadau na marafiki, unaondoka Dar es Salaam leo saa 4 asubuhi kuelekea Moshi.
Taarifa inasema MCD alifariki sekunde chache baada ya kufikishwa hospitali ya KCMC na atazikwa Kiislam dini ambayo ameitumikia mpaka kifo chake mbali na kuwa alishabadili dini mara kadhaa.
Usiku wa kuamkia leo,viongozi wa Twanga Pepeta,wadau na wasanii wa bendi mbali mbali walikutana na kuchagua kamati itakayoratibu safari ya kuelekea Moshi pamoja na mambo mengine ya kusaidia taratibu za mazishi.
Kamati hiyo ilikaa na kuwateua wafuatao kuwa wajumbe wa kamati hiyo amabao ni Omary Baraka (Mkurugenzi Msaidizi ASET), Hassan Rehani (Meneja ASET), Abdallah Dossi(Mwenyekiti Macamp ya ASET), Martin Sospeter (Meneja Mashujaa Musica), Tarsis Masela (Kiongozi Akudo Impact).
Wengine ni Deo Mutta (Katibu wa Macamp ya ASET), Rehema Kiluvia (Mdau Twanga Pepeta) na Super Nyamwela (Kiongozi Mkuu Shoo Extra Bongo) na Luizer Mbutu (Kiongozi Mkuu Twanga Pepeta) ambaye ndiye mweka hazina wa kamati hiyo.
Kwa wote watakaotaka kuchangia msiba huo kwa njia ya simu za mkononi basi wanaombwa kutuma pesa zao kupitia simu zifuatazo 0653 797976, 0762 46 00 90, 0787 090 090,namba zote zinamilikiwa na Luizer Mbutu:
Source:Saluti5.