Michezo

Unatamani kujua mapato yaliyopatikana kwa Mechi zilizowahusisha Simba na Yanga?haya hapa

By

on

yanga na simbaUnaambiwa Mechi za Ligi Kuu ya Vodacom ‘VPL’ zilizohusisha timu za Simba na Yanga na kuchezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wikiendi iliyopita zimeingiza jumla ya pesa za Kitanzania shilingi 139,850,000.
Tukianza kwa mechi ya kwanza ambapo Yanga ilicheza na Ashanti United ambapo Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ashanti United ambapo mchezo huo pambano lake liliingiza jumla ya shilingi 86,035,000 kutoka kwa watazamaji 14,261 waliokuwepo uwanjani siku hiyo
Mechi ya Simba ambayo Simba ilishinda bao 1-0 dhidi ya Rhino Rangers kutoka mkoani  Tabora mchezo huo uliingiza jumla ya shilingi 53,815,00 kutoka kwa watazamaji 9,629 waliohudhuria uwanjani.
Mgawanyo kwa mechi ya Yanga ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambapo ilikua ni shilingi13,123,983.05,gharama za kuchapa tiketi zilikua ni shilingi 2,910,300 na kila klabu ilipatiwa shilingi 20,650,211.50.
Uwanja ulilipwa shilingi 10,500,107.54, gharama za mechi sh. 6,300,064.53, Bodi ya Ligi sh. 6,300,064.53, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,150,032.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,450,025.09.
Mechi ya Simba mgawo ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 8,209,067.80,gharama za kuchapa tiketi sh. 2,910,300 wakati kila klabu ilipatiwa shilingi 12,595,211.50.
Uwanja ulilipwa shilingi 6,404,344.83,gharama za mechi shilingi 3,842,606.90, Bodi ya Ligi shilingi 3,842,606.90, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) shilingi 1,921,303.45 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) shilingi 1,494,347.13.
Source:Salehjembe.

Tupia Comments