Ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu kufariki kwa Sharo Milionea,Mama mzazi wa Marehemu Sharo Milionea amekuja na ombi kwa ajili ya waandaaji wa Movie za kitanzania hapa nchini.
Ombi hili ni juu ya kazi mbalimbali alizowahi kufanya marehemu Sharo Milionea na hazikutoka enzi ya uhai wake ambapo mama ameomba kuzisimamisha kazi zote ambazo hazijatoka na marehemu Sharomilionea alishiriki,mpaka wawasiliane na familia hiyo.
Mama mzazi wa marehemu Sharo Milionea ameingia Dar es salaam jumapili,January 26 akitokea nyumbani kwake Kijiji cha Msanga wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga mahsusi kwa ajili ya kuipromote movie itakayoonyesha maisha ya Sharo Milionea.
Wahusika kwenye movie hiyo ni pamoja na Mama mzazi huyo pamoja na wanafamilia wa Sharo Milionea ambapo ndani ya movie hiyo ya maisha ya Sharo Milionea wameigiza tangu amezaliwa hadi alipofariki November 26 2012 kwenye ajali ya gari.
Bonyeza play kumsikiliza Mama mzazi wa Sharomilionea.