Ni siku ya pili sasa katika mitandao ya kijamii hususani kwa watu mbalimbali maarufu wa nchini Kenya wamekuwa wakiendesha kampeni maalum mtandaoni ya kupinga ukamatwaji wa MaDeej’s nchini ambapo hadi sasa imeripotiwa wamekamatwa wawili.
Kampeni inayoendelea kwa sasa katika mitandao ya kijamii nchini Kenya ni #StopArrestingDjs maamuzi ambayo yamefikiwa na baadhi ya watu kufuatiwa kukamatwa kwa MaDeej’s wawili wiki iliyopita ambao ni Dj Rigz na DJ Tremor.
Maamuzi hayo yamefikiwa kama ishara ya kupinga maamuzi ya serikali ya jiji la Nairobi ambayo kwa sasa ina kamata MaDeej’s wote wanaokiuka na kupiga muziki zaidi ya saa sita usiku kwa kigezo kuwa wanachafua mazingira kwa kupiga kelele watu wakiwa wamepumzika.
Kundi la muziki la Sauti Sol ni miongoni mwa watu wanaoungana na Wakenya wengine kupinga maamuzi hayo ya jiji la Nairobi kwa kuandika ujumbe huu kupitia Twitter account yao ““As an artist, who do you turn to for support when you have new content out? As a fan, who do you go to when you’re at a party, event or in the club and want to request for your fav joint? The Dj! Therefore, let’s all join the #StopArrestingDjs thread and show support for our DJs.