Mume wa zamani wa muimbaji wa Injili Flora Mbasha amlilia mtoto wake mtandaoni ikiwa ameandika machungu anayoyapata kutomuona mtoto wake kwa zaidi ya miaka miwili toka aachane na mke wake na hivyo mke wake kuolewa na mwanaume mwingine.
Ikiwa ni siku ya wanawake duniani February 8,2018 Emmanuel Mbasha alitumia mtandao wake wa instagram kumtaka mke wake wa zamani kumruhusu kumpa nafasi ya kumuona mwanae kwa sababu kama ameshindwa kutumikia sheria iliyotolewa na mahakama basi atatumia mtandao wa kijamii.
“Happy women’s day ila ulinizalia mtoto mzuri sana kwa hilo nakushukuru mno nimemmiss lizy sana unipage basi mtoto unaninyima kabisa daaah karibu mwaka wa 2 inaelekea 3 sasa sijamwona mtoto duuu mie baba ake tu ila nakuomba hata siku moja moja nifurahie maisha na dogo basi daaah”
“Nakuomba nimwone mwanangu Lizy, najua hata mtoto amenimiss sana mana ameondoka kwangu akiwa mkubwa na nimemlea tangu mtoto ila anashindwa kuongea tu ila najua ananikumbuka sana.”
“Mahakama iliamua mtoto akae na mama ila niwe namwona mtoto, sasa unapingana na mahakama sitaki povu nimeongea na mzazi mwenzangu x wife, mke wa mtu njia za kawaida naona imeshindikana unakaza sana aise sasa inabidi nikuombe insta”
Ulipitwa na maneno ya Majizzo kwa Lulu “Utakuja kuisoma one day”