Mwanamitindo wa Kitanzania Millen Magese ambaye kwa sasa makazi yake yapo nchini Marekani anazidi kuitangaza na kuipeperusha bendera ya Tanzania popote pale aendapo hii ni kutokana na kuhudhuria mikutano mikubwa ikiwemo Umoja wa Mataifa na kuongelea masuala ya ugonjwa wa Endometriosis.
Millen Magese alipata nafasi ya kuhutubia katika chuo cha Harvard ambacho ni maarufu nchini Marekani March 3 ,2018 , ambapo inakuwa ni mara ya kwanza kuchaguliwa kuongelea juu ya ugonjwa wa Endometriosis ambao umekuwa ni tishio kubwa kwa wanawake na amekuwa akifanya hivyo katika nchi mbalimbali ifikapo mwezi wa tatu kila mwaka.
Jina la Millen lilizidi kuchukua headlines baada ya kufanikiwa kupata mtoto wake wa kwanza, kwani inaripotiwa kuwa kwa kiasi kikubwa ugonjwa wa Endometriosis uliyokuwa unamsumbua Millen kwa miaka mingi unaweza kusababisha mwanamke kushindwa kushika mimba na kupata mtoto.
Chuo cha Harvard ni moja kati ya vyuo vikubwa Duniani kilichopo Marekani ambacho kilianzishwa mwaka 1636 na watu maarufu na wakubwa mbalimbali duniani wamewahi kusoma chuo hicho kama Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama, muigizaji Matt Damon na John F. Kennedy.
Ulipitwa na gumzo mtandaoni, Dogo Janja kapaka lipstick kavaa nguo za kike??