Kuna aina nyingi za viumbe duniani, vingine vya kustaajabisha. Ayo TV na millardayo.com inakuletea orodha ya aina tano za mbwa wa ajabu zaidi duniani.
1. Inca Orchid
Aina hii inapatikana nchini Peru. Ni aiana ya mbwa ambao hawana manyoya kabisa, ngozi zao ni kama za binadamu. Aina hii ya mbwa ni adimu sana na inaelezwa kuwa wapo mbwa na aina hii 1000 tu duniani.
2. Lundehund
Hawa ni aina ya mbwa wanaopatikana nchini Norway. Kwa kawaida mbwa huwa na vidole vinne lakini mbwa aina hii wana vidole sita.
3. Puli
Mbwa hawa wanapatikana nchini Hungary. manyoya yao ni mfano wa kamba zilizofungamana na ndio tabia inayowafanya kuwa wa kipekee.
4. Catahoula Cur
Aina hii ya mbwa hupatikana Louisiana nchini Marekani. Utofauti wao ni kwamba wanauwezo wa kupanda miti, jambo ambalo aina nyingi za mbwa haziwezi. Macho ya mbwa hawa huweza kuwa na rangi tofauti, lakini pia inawezekana kila jicho la mbwa huyu kuwa na rangi zaidi ya moja.
5. Shar-Pei
Hii ni aina ya mbwa ambayo inapatikana China. Mbwa hawa ngozi zao zina makunyazi, na wakiwa wadogo mwili mzima huwa na mikunjo hiyo lakini wakiwa wakubwa mikonjo hiyo inahamia kichwani. Inaelezwa kuwa ngozi hii inawaweka mbwa hawa salama kwani, kama kuna mnyama anataka kuwadhuru mara nyingi huishia kuvuta ngozi tu.
Kinachatokea kwenye ubongo ukinywa pombe na mgawanyiko wake mwilini