Leo March 29,2018 story ya entertainment nayokusogezea ni inayomhusu muigizaji wa Bongo Movie Shamsa Ford ambapo kupitia ukurasa wake wa instagram amewashauri wasanii nchini kuhusiana na kufanywa kuwa ambassadors wa bidhaa fulani wanatakiwa kuwa watu wanaojielewa na sio tu kwasababu ya umaarufu walionao ndio utawapatia nafasi kama hizo.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Shamsa Ford ameandika……>>>“Morning my people. Naona tu watu wanalalamika kwanini madili yanawapita mastar wa bongo na wageni ndo wanapata nafasi hiyo mimi nina mtazamo tofauti kabisa kabla ya kuanza kumtafuta mchawi ni nani ni bora kwanza tukajikagua wenyewe kwanza nina uhakika kila biashara ina condition zake na kila biashara inahitaji faida”
“Hakuna mfanyabiashara atayekubali kumchukua STAR wa bongo kisa uzalendo tu halafu apate hasara. Tusipinge ukweli sisi wenyewe baadhi ya wasanii tumevunja uaminifu kwa wafanyabiashara wakubwa kutokana na matendo yetu.” -Shamsa
“Unapozungumzia kuwa ambassador unazungumzia kubeba brand ya mtu, sasa ni nani anaetaka kuchafua brand yake ibebwe na mtu asieeleweka, swala sio kujulikana tu ila unajulikana vipi!?” -Shamsa
“Maana kama jamii inakudharau hata hiyo bidhaa unayoibeba itadharaulika. kikubwa tujifunze, swala sio kujulikana ila swala ni kuwa unajulikana vipi!? Watu wanakutambua kwa lipi kisha akili kichwani mwako ni vizuri tumeumia sasa tujipange na kufukiaa mashimo yaliyotoboka ili na sisi tueshimike na kuthaminika niliowakera mnisamehe tu lazima tuishi kwa kuambiana ukweli”
“Nilipokuwa Mwanamuziki nilikuwa vizuri sana kuliko nilivyo Mbunge” Prof. Jay