Kutoka nchini Kenya, vijiji 200 ambavyo viko magharibi mwa nchini hiyo wanaripotiwa kupata ‘neema’ ya kupokea Dola za Marekani 22 sawa na Shilingi za Kitanzania 52,800 kila mwezi.
Pesa hii inaelezwa kuwa ni ya kujikimu kwa familia zao kila mwezi na pesa hizi hutumwa kwa njia ya simu, lengo kuu ikiwa ni kuboresha maisha ya wakazi wa vijiji hivyo.
Pesa hiyo hutumika kwa matumizi ya kilimo, biashara, ada za shule, ujenzi na hata katika afya. Hatahivyo baadhi ya watu wamekosoa utaratibu huo wakisema kuwa unawalemaza wakazi hao kutokufanya kazi kwa bidii na kujiingizia kipato wenyewe.
Misaada hiyo ya pesa inatolewa na shirika moja linalojulikana kama GiveDirectly.
Mrisho Mpoto amwambia Steve Nyerere “Punguza gubu ndugu yangu”