Wachekeshaji maarufu nchini ambao wamepata umaarufu kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram na Facebook, Ebitoke na Bwana Mjeshi wanao simamiwa na Timamu wamekua miongoni mwa wasanii wachache kutokea Africa kujisajili kwenye mtandao wa IMDb.
IMDb ni mtandao unaoweka taarifa mtandaoni zinazohusu mastaa wa kubwa wa filamu pamoja na filamu kubwa, zikiwemo tamthilia zinazoruka kwenye Television mbalimbali kubwa ulimwenguni. Ebitoke na Bwana Mjeshi baada ya kujisajili waliamua kupost kwenye Instagram zao huku wakiwa ni miongoni mwa waigizaji wachache sana kutokea bongo na staa mwingine ambaye yupo ni Idriss Slutani.
Baada ya post hiyo millardayo.com na Ayo tv ikamtafuta kuzumgumzia hilo msikilize hapa chini kwa ku-Bonyeza PLAY
MSIBA WA MASOGANGE: BELLE 9 AMESHINDWA KUONGEA MSIBANI
Mzee Majuto azidiwa, arudishwa tena Hospitali kwa tatizo jingine