Dunia ikiwa inaadhimisha Siku ya Malaria duniani jana April 25, 2018, Shirika la Afya duniani (WHO) limeeleza kuwa malaria bado ni tatizo kubwa duniani na changamoto kubwa ikiwa maambukizo, udhibiti na tiba, hasa barani Afrika.
Ripoti ya shirika hilo inaeleza kuwa kwa mwaka 2016 pekee, kumekuwa na maambukizi Milioni 216 ya malaria na kusababisha vifo 445,000 dunia nzima.
Kuanzia July, hakutakua na Parking za watu binafsi Mwanza.
Na katika takwimu hizo, inaelezwa kuwa asilimia 90 ya wanaougua malaria na asilimia 91 ya vifo vyote vinavyosababishwa na malaria vilitokea barani Afrika.
Nchini Tanzania inaelezwa kuwa asilimia 93 ya raia wako hatarini kupata maambukizi hayo, huku Kenya ikiwa na asilimia 70 ya idadi ya watu walioko hatarini kupata malaria.
Fatma Karume: Kwa kila watu 25,000 kuna mwanasheria mmoja