Wiki kadhaa zimepita baada ya kampuni ya Facebook ikabiliwe na kashfa ya matumizi mabaya ya taarifa binafsi za wateja wa mtandao huo zaidi ya Milioni 50 kulikofanywa na kampuni ya Uingereza ya Data Analytica iliyokuwa na uhusiano na timu ya kampeni ya Rais Donald Trump mwaka 2016
Hatahivyo tofauti na ilivyodhaniwa, Facebook imeripoti kuwa mauzo ya kampuni hiyo yameongezeka kwa asilimia 50 tangu kashfa hiyo itokee na kutingisha kampuni hiyo.
Kuanzia July, hakutakua na Parking za watu binafsi Mwanza.
Inaelezwa kuwa mapato ya kampuni hii yamepanda hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 11.9 sawa na shilingi Trilioni 28.5 katika kipindi cha mwezi January hadi March mwaka huu 2018 ukilinganisha na Dola bilioni 8 miaka iliyopita.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mark Zuckerberg ameeleza kuwa “pamoja na kukabiliwa na changamoto, biashara yetu imeanza vizuri mwaka 2018 na tunachunguza upya wajibu wetu”.
Fatma Karume: Kwa kila watu 25,000 kuna mwanasheria mmoja