Picha ya kwanza na baadhi ya nyingine zinazofata ni za Mirror, msanii ambae yuko chini ya kampuni ya mwigizaji Wema Sepetu.
Huu ni mwaka wa sita toka kuanzishwa kwa A.M Records ambayo Producer Maneke na rafiki yake mkuu aitwae Abuu waliianzisha kwa mtaji wa dola elfu 6 za Kimarekani ambazo ni zaidi ya milioni tisa za Kitanzania kwa sasa.
Baada ya kusumbuka na computer pamoja na vifaa vingine vya kuungaunga, wawili hawa waliketishwa chini na Baba mzazi wa Abuu ambae walimwambia wanachotaka wao ni kufanya muziki, ndio akawapa huo mtaji.
Mwigizaji Kajala ambae ni rafiki wa Wema Sepetu, alijitokeza kumpa support Mirror akisindikizwa na rafiki zake
Huyu ni msanii mpya wa AM Records anaitwa Keizer.
Mwigizaji Riyama Ally ni miongoni mwa waliopanda kwenye stage na kutoa support ya kucheza na Jux baada ya kuguswa na alichokua anaimba.
Quick Rocka ndio akamaliza show, hao ni baadhi tu ya walioonekana kwenye stage ila kuna list nyingine itakuja na AyoTV soon mtu wangu.