Bunge la Katiba bado linaendelea 104.4 Dodoma na miongoni mwa watu waliopata fursa ya kuwepo kwenye bunge hili ni wasanii wa Tanzania ambapo jumla ya wasanii 12 wakiwa pamoja na viongozi toka Shirikisho la muziki,Shirikisho la Filamu,Shirikisho la Sanaa za ufundi na Mtandao wa Wanamuziki Tanzania hawa ni miongoni mwao waliowawakilisha wenzao Dodoma.
Sababu kubwa ya wasanii hao kuelekea Dodoma na kuwepo kwenye mfululizo wa mikutano na wabunge mbalimbali ni kuwashawishi wabunge waunge mkono vipengele viwili ambavyo wasanii wanavitaka katika Katiba
Vipengle wanavyohitaji wasanii ni pamoja na
- Kundi la wasanii kutambuliwa katika Katiba kama vile walivyotambuliwa Wakulima, wafugaji, wavuvi na wafugaji walivyotajwa.
-
Milliki Bunifu kwa kiingereza Intellectual Property ambamo ndani yake kuna Hakimiliki itajwe rasmi katika Katiba hili litawezesha sheria mwafaka zitungwe katika kuendeleza sanaa na kulinda kazi za sanaa na kazi za ubunifu. Kundi hili limepokelewa vizuri sana na wabunge wote lililokutana nao.
Picha:Mzee kitime.