Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amelieleza Bunge kuwa hakubaliani na kitendo cha Serikali kuweka mapendekezo ya kufuta ushuru wa asilimia 65 ya pesa zitokanazo na mauzo ya zao la korosho ghafi nje ya nchi (export levies) jambo ambalo amedai ni ajenda itayokwenda kuiua CCM katika mikoa ya kusini.
“Haya mnasema kuna matumizi mabaya ya fedha kwenye huu mfuko hivi dawa yake ni kuufuta? Dawa yake ni kuchukua hela? Mbona hazina kuna hati chafu hatusemi? NO… !!tusiende huku, haya ni maisha yetu you want to kill us? Serikali kuweni na huruma kidogo na niwaambie mapendekezo haya yanakwenda kuiua CCM kusini” –Nape Nnauye
Mbowe alivyofika mahakamani Kisutu baada ya kufiwa na Kaka yake