Watanzania Laigwanani Mollel na Ziporah Godfrey Mollel
walioshiriki michuano ya soka kimataifa ya Football for Friendship
(F4F) wameondoka Urusi kurejea Tanzania wakiwa na ndoto ya
kuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Dunia miaka ya baadae.
Michuano hiyo ya F4F ilishirikisha watoto wenye miaka 12 kutoka nchi
211 na imefanyika kwa mwaka wa sita tangu kuanzishwa kwake, Laigwanani na Ziporah wakitokea akademi ya Lengo Football ya Arusha
na wameondoka Urusi kurejea Tanzania.
“Niliwakilisha vizuri Tanzania kwa kupeperusha bendera ya taifa kwenye sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia 2018, ilikuwa kabla ya
mechi ya ufunguzi ya Urusi na Saudi Arabia, nilikuwa na uchovu sana baada ya kazi ya siku ile lakini naamini nimepata hamasa ya kuiwakilisha nchi yangu katika Kombe la Dunia siku zijazo kwa mimi mwenyewe kucheza uwanjani”>>> Laigwanani.
“Nitakua na faraja sana kwa sababu Tanzania haijawahi kufuzu katika fainali za Kombe la Dunia, hivyo nitakuwa ni mimi ninaye iwakilisha nchi yangu, nitajisikia ujasiri na nitaiwakilisha nchi yangu vizuri na najua katika mawazo yangu kuwa siku moja Tanzania itakuwa hapa katika fainali za Kombe la Dunia”>>>> Ziporah
Program hii ya Kijamii ya F4F ni programu ya kijamii inayojumuisha
siku tatu za mafunzo ya soka na kila timu kati ya timu 32 kutoka
duniani kote zilizipewa majina ya wanyama walio hatarini kupotea.
Timu zilizoundwa zilijumuisha wachezaji kutoka kila pembe ya dunia,
kutoka mataifa makubwa na wadogo bila kujali, dini, tamaduni na
ushawishi wa kisiasa na wa kiitikadi.