Leo August 1, 2018 tunayo story kutokea kwa upande wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambapo umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wanatarajia kuwa na shahidi mwenye utaalamu wa Elektroniki ili achambue Email katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake.
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo imekuja ili kuendelea na ushahidi kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Mzigama.
Swai amedai kuwa wanaiomba mahakama iruhusu kusimamisha ushahidi wa Kidao kwa muda ili wamlete shahidi mwingine ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Elektroniki ili aweze kuchambua mawasiliano ya Email katika kesi hiyo.
Swai amedai kuwa hatua ya kutaka kumleta mtaalamu huyo inatokana na kutaka kuwasilisha kielelezo cha Email kama ushahidi ambapo mawakili wa pande zote waliipitia.
“Shahidi wa sasa hana utalaamu wa email, hivyo tunataka tumlete mtalaamu wa Elektroniki ili aichambue email na aweze kuitoa mahakamani,”.ameeleza Swai.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi August 14 na 15,2018 ili kusikilizwa mfululizo.
Washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine, Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga.
Washtakiwa hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 29,2017, wakikabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha Dola za Marekani 375,418.
Katika kesi hiyo, Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 28 ya uhujumu uchumi ikiwamo kughushi na utakatishaji wa fedha Dola za Marekani 375,418.
Katika kesi hiyo Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 28 huku wenzake wakikabiliwa na makosa yasiyozidi manne.