Leo August 4, 2018 kundi la muziki wa bongofleva la Navy Kenzo wame-launch Navy Kenzo foundation ambayo ni project yao ya kwanza ambayo itajishughulisha na masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kutoa misaada mbalimbali na kuanzisha Navykenzo Cup ikiwa ni kwa lengo la kuwasaidia vijana wenzao kunyanyua na kukuza vipaji kupitia sector hii nyingine ambayo ni tofauti na muziki.
Navykenzo wamezindua Foundation hiyo na kwa mara ya kwanza wametangaza Rasmi kuanza na Mchezo wa Soka na kuanzisha NAVY KENZO CUP ambapo mashindano yatakuwa yanafanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers na itaanza na Timu nane na wameanza na mkoa wa Dar es Salaam kisha baada ya Hapo wataelekea kwenye Mikoa Mingine, huku Timu za Dar ambazo zitashiriki zitakuwa 8 Pekee.
EXCLUSIVE:’Sikuwahi kuwaza kuteuliwa nafasi kama hii’- DC JOKATE MWEGELO
Seven Mosha kaweka wazi Ugonjwa unaomsumbua Ommy Dimpoz