Baada ya siku kadhaa kusambaa kwa taarifa kuwa hali ya Ommy Dimpoz sio nzuri na hivyo kurudishwa hospitalini nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi mashabiki walipata hofu kutokana na yeye kutozungumza chochote.
Kwa mara ya kwanza kupitia snapchat story ya Ommy Dimpoz ameweka wazi kuhusiana na hali yake ya sasa baada ya taarifa kusambaa kuwa yupo ICU na kusema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri na ana imani kuwa atavuka kipindi hiki kigumu na anawashukuru wale wote waliomjulia hali.
Ommy Dimpoz aliandika “Asanteni sana sana kwa msgs zen Alhamdulilaah naendelea vyema sana Insha Allah kwa uwezo wake Allah nitavuka kipindi hiki kigumu Shukhrani”
Sababu za Wolper kukatwa kuwa Jaji Miss Lake Zone ”HAKUNA UMAARUFU”