Mkali wa Hip Hop Jay Z ashika nafasi ya kwanza kwenye list ya wasanii wa Hip Hop wanaoingiza mkwanja mrefu kwa mwaka 2018 na ametajwa katika jarida la Forbes World’s Highest Paid Hip Hop Acts na hii ni baada ya kumpindua P.Diddy.
P Diddy ambae alishika nafasi ya kwanza kwa zaidi ya miaka miwili ameshuka hadi nafasi ya pili kwa kupinduliwa na Jay Z ambaye anatajwa kuingiza thamani ya dola za Kimarekani Milioni 76.5 sawa na zaidi ya Bilioni 180 za Kitanzania kutokana na pato lake kuonekana kukuwa kuanzia 2017 -2018.
Wakali wengine wanaoikamilisha list hiyo ni pamoja Kendrick Lamar, Drake, J Cole, Nas na wengine wengi na inatajwa kuwa Jay Z amefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya ziara yake ya muziki On The Run II(OTRII) akiwa na mke wake Beyonce ambayo bado inaendelea kumuingia mkwanja mrefu zaidi.
Leo kwa mara ya kwanza Ommy Dimpoz katuonesha alivyokuwa ICU