Msanii Dogo Janja amewashangaza wengi baada ya ujumbe aliouandika kupitia ukurasa wake wa instagram ikiwa ni siku moja imepita tokea asherekee siku yake ya kuzaliwa akiwa hospitalini baada ya kuugua ghafla.
Maswali yaliibuka kwenye mitandao ya kijamii baada ya mke wake Irene Uwoya kutoonekana hospitalini akiwa nae, huku wengi kujiuliza kama ana taarifa kuhusiana na Dogo Janja kulazwa hospitalini? au tetesi hizi zina ukweli wowote kuwa wameachana?
Leo September 17,2018 Dogo Janja kaibuka kwenye mtandao wa instagram na kuandika “BADO NA IMANI YOTE NA PITIA🙏🏻 😌” hii ni baada ya kupost picha ya mke wake Irene Uwoya, wengi wameanza kuamini tetesi zinazoendelea kuwa Janja na Irene hawako katika maelewano mazuri kwa sasa.
Mashahidi 25 kesi Mwanafunzi aliefariki kwa viboko, Mahakama yaamuru