Inaonekana jina la Tanzania sweetheart bado linatrend kwenye mitandao ya kijamii, hii ni kutokana na kila mtu kutoa mawazo yake kuhusiana na jina hilo huku wengine wakisema kuwa ni nick name na mtu yeyote anaweza kuitwa au kujiita jina hilo.
Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga naye amaeonekana kutumia jina hilo la Tanzania sweetheart na hii ni baada ya kutumia ukurasa wake wa instagram na kuandika ujumbe na kusema kuwa anasikitishwa na wanaume wa Dar kugombania kuita wake za watu ‘Tanzania sweetheart” na huku wake zao wanawaangalia tu.
“Tanzania sweetheart, mama wa watoto 3 hapo camera ya nokia 9300. Wababa wa Dar Mungu atusamehe tunagombania kuita wake za watu Tanzania sweetheart huku mkeo anakuangalia “Pumbavu zetu” kama nawaona mnavyo screenshot”
Jina la Tanzania sweetheart linaonekana kugombaniwa kutokana na mashabiki kudai kuwa Wema Sepetu ndio mmiliki wa nick name hiyo na wengine wakidai kuwa mrembo Hamisa Mobetto ndie anayestahili kuitwa Tanzania sweetheart.
RADO: Rais akilala, akiamka ni muda wa BONGO MOVIE’