Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu miaka 28 jela aliyekuwa mfanyakazi wa benki ya NMB, Mtoro Midole na Daudi Kindamba baada ya kuisababishia hasara benki hiyo ya Sh.Bilioni 1.03.
Hukumu hiyo imeandaliwana n Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa na kusomwa na Hakimu Mkuu, Wanjah Hamza.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Wanjah chini ya sheria ya kanuni ya adhabu aliamuru washtakiwa hao mbali na adhabu ya vifungo hivyo pia walipe kiasi cha Sh.Bilioni 1.03 ambacho wanadaiwa kusababisha hasara kwa NMB.
Kwa upande wa mshtakiwa ,John Kikoka ambaye alikuwa miongoni mwa washtakiwa hao, alimuachia huru baada ya mashahidi 21 walioitwa na upande wa mashtaka kutoa ushahidi kwenye kesi hiyo ya jinai namba 118 ya 2014, kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake pasipo kuacha shaka.
Katika kesi hiyo, washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 13 ya kula njama, wizi, kusababisha hasara na utakatishaji wa fedha ambayo kila mshtakiwa alikuwa akikabiliwa na mashtaka mawili.
Mkurugenzi TAKUKURU “Wakurugenzi sita Mahakamani kwa Uhujumu uchumi”