Waziri mwenye dhamana ya kusimamia sanaa nchini Dr Harrison Mwakyembe amemteua msanii Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA kuwa sehemu ya wajumbe wa bodi ya BASATA.
Imekuwa ikidaiwa kuwa Baraza la Sanaa la Taifa BASATA limekuwa na mapungufu huku wengine kwenda mbali zaidi na kuiomba serikali iwaoe uongozi wasanii wenyewe wasimamiane.
Kwa vilio hivyo vya muda mrefu kutoka kwa wasanii serikali imeonekana kuvisikia na kuamua kuwapa nafasi za uongozi wasanii wenyewe ikiwemo na muigizaji wa Filamu nchini Single Mtambalike maarufu kama Richie.
Ya Wema yamfikia Esha Buheti, Wolper aingilia kati