Jarida la Billboard limemtaja muimbaji wa Pop Ariana Grande kuwa mwanamke wa mwaka 2018( Billboard 2018 Woman of the Year) na hivyo kukabidhiwa tuzo ya heshima December 6,2018.
Ariana Grande ameweza kushikilia chart za Billboard 200 kwa kushika nafasi ya kwanza mara tatu ikiwemo na album yake ya ‘Sweetner’ ambayo ilikaa nafasi ya kwanza mwezi wa August 2018 na kushika rekodi ya kuwa msanii wa nne wa kike kuingiza nyimbo nyingi kwenye chart za Billboard Hot 100.
Mkuu wa maudhui ya Billboard Ross Scarano amesema kuwa Ariana Grande anastahili kupata tuzo hiyo kutokana na kutoa aina ya muziki ambao jamii inanufaika nao ikiwa na kujiamini na kusimama peke yake. Ugawaji wa tuzo hizo unatarajiwa kufanyika usiku wa December 6,2018 katika sherehe za Woman In Music jijini New York.
Ariana Grande ataungana na wakali kama Selena Gomez, Madonna, Lady Gaga na Taylor Swift ambao pia waliwahi kukabidhiwa tuzo hiyo kutokana na mchango mkubwa wa muziki wanaoufanya.
EXCLUSIVE: Miss Tanzania afunguka alivyotabiriwa na Mchungaji kushinda Miss World