Leo November 8, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amekutana na Wataalamu wa Moyo kutoka nchini Israel wakiongozwa na Balozi wa Isarel pamoja na Madaktari wa Hospitali ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Madaktari na Wataalamu kutoka Israel wapo nchini kwaajili ya kuwatibu Watoto 51 wenye matatizo ya Moyo. Nimekusogezea Mambo 7 aliyozungumza Rais Magufuli mbele ya Wataalamu hao.
“Mtu mwenye Moyo safi maisha yake kazi yake inakua kuokoa maisha ya wengine, nawashukuru sana Madaktari kutoka Israel” Rais Magufuli Ikulu akiongea na Wataalamu wa matibabu ya Moyo kutoka Israel na Tanzania.
“Mtu mwenye Moyo safi maisha yake kazi yake inakua kuokoa maisha ya wengine, nawashukuru sana Madaktari kutoka Israel” Rais Magufuli Ikulu muda huu akiongea na Wataalamu wa matibabu ya Moyo kutoka Israel na Tanzania. #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/CvexdWwwfV
— millardayo (@millardayo) November 8, 2018
“Nimeandika barua ambayo nitakukabidhi umpelekee Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuonyesha appreciation yangu, najua hii barua itamfikia ili kuonesha kazi nzuri mliofanya” Rais Magufuli akimkabidhi Balozi wa Israel barua ampelekee Waziri Mkuu wake.
“Nimeandika barua ambayo nitakukabidhi umpelekee Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuonyesha appreciation yangu, najua hii barua itamfikia ili kuonesha kazi nzuri mliofanya” Rais Magufuli akimkabidhi Balozi wa Israel barua ampelekee Waziri Mkuu wake. #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/LzkwBZDDgM
— millardayo (@millardayo) November 8, 2018
“Tanzania itaendelea kushirikiana na Israel, itashirikiana na Marekani na ndo maana katika Awamu hii niliamua kufungua Ubalozi kwa makusudi wa Israel, urafiki kati ya Tanzania na Isarel utaendelea kudumu” Rais Magufuli
“Tanzania itaendelea kushirikiana na Israel, itashirikiana na Marekani na ndo maana katika Awamu hii niliamua kufungua Ubalozi kwa makusudi wa Israel, urafiki kati ya Tanzania na Isarel utaendelea kudumu” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/gLJop8TlYE
— millardayo (@millardayo) November 8, 2018
“Naomba mtenge siku mbili hata tatu tuwapeleke Serengeti Nationa Park au Ngorongoro mkakae hamtalipa chochote ofa itatolewa na Serikali lakini mkiona haiwezekani kwa sasa ofa itabaki palepale mnaweza mkapanga ratiba nyingine mkaja” -Rais Magufuli
“Naomba mtenge siku mbili hata tatu tuwapeleke Serengeti Nationa Park au Ngorongoro mkakae hamtalipa chochote ofa itatolewa na Serikali lakini mkiona haiwezekani kwa sasa ofa itabaki palepale mnaweza mkapanga ratiba nyingine mkaja” -Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/Ijx4fWs0D4
— millardayo (@millardayo) November 8, 2018
“Tenda ya kusambaza madawa ktk nchi za SADC tumepewa Tanzania” -Rais Magufuli
“Tenda ya kusambaza madawa ktk nchi za SADC tumepewa Tanzania” -Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/DaWE2aUeJe
— millardayo (@millardayo) November 8, 2018
“Niwaombe Madaktari na Wataalamu kutoka Israel mkija msije tu kwa masuala ya Udaktari siku nyingine mnaweza mkaja kwa masuala ya kufurahi, mnaenda Serengeti National Park, Ngorongoro na maeneo mengine ambayo ni ya kuvutia” Rais Magufuli
“Niwaombe Madaktari na Wataalamu kutoka Israel mkija msije tu kwa masuala ya Udaktari siku nyingine mnaweza mkaja kwa masuala ya kufurahi, mnaenda Serengeti National Park, Ngorongoro na maeneo mengine ambayo ni ya kuvutia” Rais Magufuli #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/bJl9sgxEnp
— millardayo (@millardayo) November 8, 2018
“Ndugu zangu mliokuja kushughulikia Watoto 51 mtakaporudi Israel msiisahau Tanzania, mjue tunahitaji misaada yenu, kama kuna ndugu zetu Israel wanaweza kutoa donation za aina yoyote ktk Hospitali zetu itakuwa vizuri, mjue Tanzania inawahitaji” Rais Magufuli
“Ndugu zangu mliokuja kushughulikia Watoto 51 mtakaporudi Israel msiisahau Tanzania, mjue tunahitaji misaada yenu, kama kuna ndugu zetu Israel wanaweza kutoa donation za aina yoyote ktk Hospitali zetu itakuwa vizuri, mjue Tanzania inawahitaji” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/IJND7vAUSo
— millardayo (@millardayo) November 8, 2018