Unaambiwa Dubai kuna club za usiku za aina mbalimbali zikiwemo za kawaida na za wale matajiri sana na pia kuna club za watu maarufu kama Movida na Mahiki ambazo zinakuwa na matawi mbalimbali duniani.
Ni sehemu ambako kuna club za usiku zinazomilikiwa na Madesigner kama Roberto Cavalli na Georgio Armani ambapo kwenye night club hizi za matajiri, shilingi milioni 10 za Kitanzania kuachwa kwenye meza sio stori yani.
Club nyingi huanza kujaa kuanzia saa sita na nusu usiku na ni sharti kwamba kila club ya usiku ifungwe kila ifikapo saa tisa kamili ili kuruhusu watu kwenda kupumzika na kujiandaa na shughuli za asubuhi yake.
Unaambiwa baadhi ya club hizi za usiku huko Dubai, haziruhusu Wanaume kuingia bila Wanawake, yani ni lazima kuwe na Mwanamke hata mmoja kwenye kundi la Wanaume, wanaamini Wanaume hutumia pesa nyingi zaidi wakizungukwa na Wanawake lakini pia inasaidia kuepuka vurugu.
Club zote za Dubai ambazo zinatakiwa kuwa zimefungwa kila inapofika saa tisa kamili usiku na watu kuamriwa kutoka nje, huwa zinaruhusiwa kuongeza saa moja na kufungwa saa kumi lakini kwenye zile sikukuu muhimu tu.
Club hizi za usiku haziruhusiwi pia kuuza vilevi kwenye sikukuu muhimu za kidini ambapo siku hizi maalum zina jina maarufu la ‘dry night’
Club nyingi za matabaka ya kati hadi juu huwa na dress code, yani haziruhusu mtu kuingia akiwa kavaa kofia, raba za michezo, kaptula n.k
Unaambiwa kwenye club za Madesigner wakubwa wa dunia kama Armani, Cavalli, Mahiki, Movida, Cristal by people ni lazima ufanye reservation kwanza ndio uweze kuingia ambapo bei ya chini kabisa ya kumiliki meza moja usiku huo ni milioni moja ya Kitanzania.
Club nyingi huonyesha dakika ukutani muda mfupi kabla ya kufungwa ili kuwakumbusha wateja kwamba time ya kufunga imekaribia.
Club za matabaka ya juu pia wakati mwingine zinatumika kama sehemu ambayo matajiri huenda kuonyesha magari yao ya kifahari.
Kunazo club zinazocheza muziki wa mataifa mbalimbali ambapo kuna club za Wahindi na mataifa mengine ambayo yana raia wengi wanaoishi na kufanya kazi kwenye nchi hii.
Asante kwa Watanzania Terry Sudi pamoja na Said Mohamed waliofanikisha kuyajua mengi kuhusu Dubai.
Kwa stori kama hizi na nyingine za Tanzania kwenye siasa, muziki, michezo, breaking news na mengine ungana na mtu wako wa nguvu kwenye facebook twitter na instagram kwa jina hilohilo la millardayo ili kuwa karibu zaidi na kila tukio linalotokea.