Simba SC imeanza mchezo wake wa kwanza hatua ya Makundi ya CAF Champions League dhidi ya JS Saoura ya Algeria, Simba SC leo ilikuwa inacheza na timu ambayotajwa kuwa changa katika michuano ya CAF Champions League lakini uimara wa Simba uliwasaidia kupata matokeo chanya katika game hiyo.
Simba SC ikiwa na faida ya uwepo wa mashabiki wake uwanjani wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0, magoli ya Simba SC yakifungwa na Emmanuel Okwi dakika za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko, ila kuumia kwa John Bocco na kuingia kwa Meddie Kagere dakika ya kulifanya Simba iongeze magoli mawili dakika ya 51 na 67.
Ushindi huo sasa unaifanya Simba SC kuwa timu ya kwanza kutoka Kundi D kuvuna point tatu wakati wakiwa wanasubiria kujua matokeo ya game ya Al Ahly dhidi ya AS Vita inayochezwa usiku huu, Simba SC sasa itasafiri kwenda Congo January 19 kucheza mchezo wake wa pili dhidi ya AS Vita wakati Al Ahly watakuwa Algeria January 18 kucheza dhidi ya JS Saouro.
Mpenja katangaza goli kabla ya kona kupigwa, ataomba kutotangaza game za timu yake